WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAOMBA ZAIDI YA TSH. BILIONI 2095


Wizara ya Mifugo na Uvuvi yaomba kuidhinishiwa kiasi cha Shilingi Shilingi 295,920,933,000. hayo yakiwa ni Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo katika mwaka 2023/2024.


Ombi hilo Limewasilishwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega May 2, 2023 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24.


"Katika mwaka 2023/2024, Wizara inaomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya jumla ya Shilingi 295,920,933,000.00. Kati ya fedha hizo, Shilingi 112,046,777,000.00 ni kwa ajili ya Sekta ya Mifugo (Fungu 99) na Shilingi 183,874,156,000.00 kwa ajili ya Sekta ya Uvuvi (Fungu 64). Mchanganuo wa fedha zinazoombwa kwa kila Fungu ni kama ifuatavyo" Alisema Mhe. Ulega 


"Wizara inaomba kutumia jumla ya Shilingi 112,046,777,000 kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya Sekta ya Mifugo. Kati ya fedha hizo, Shilingi 50,122,670,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 61,924,107,000 ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo ambapo Mgawanyo  wake ukiwa ni Fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi 50,122,670,000, Mishahara Shilingi 23,939,807,000, Matumizi Mengineyo (OC) Shilingi 26,182,863,000, Fedha za Matumizi ya Maendeleo: Shilingi 61,924,107,000, Fedha za Ndani, Shilingi 56,592,173,000, Fedha za Nje, Shilingi 5,331,934,000. " Mhe. Ulega.


Pia katika Sekta ya Uvuvi Wizara imeomba jumla ya Shilingi 183,874,156,000 kwa ajili ya kutekeleza majukumu katika mwaka 2023/2024 ambapo Kati ya fedha hizo, Shilingi Shilingi 49,462,296,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 134,411,860,000 ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo.


"Mchanganuo wake ukiwa ni Fedha za Matumizi ya Kawaida: Shilingi 49,462,296,000, Mishahara ni Shilingi 15,368,951,000, Matumizi Mengineyo (OC) ni Shilingi 34,093,345,000, Fedha za Matumizi ya Maendeleo Shilingi 134,411,860,000,  Fedha za NdaniShilingi 110,682,025,000, Fedha za Nje Shilingi 23,729,835,000" Alisema Mhe. Ulega

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA