TPDC YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA KUHUSU MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI EACOP


Mratibu wa Mradi wa EACOP kitaifa, Asiadi Mrutu akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP

Na Sumai Salumu & Kadama Malunde - Shinyanga

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi amewataka waandishi wa Habari kuandika habari sahihi na kutoa elimu sahihi kwa wananchi kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).


Akizungumza leo Jumanne Septemba 26, 2023 wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) yaliyolenga kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa EACOP, Samizi amesema waandishi wa Habari wana jukumu kubwa la kutoa taarifa sahihi kwa wananchi ili kujua faida za mradi huo.

“Nitoe wito kwa waandishi wa habari muandike taarifa na habari sahihi kuhusu mradi, ili wananchi waweze kuufahamu mradi huu, tunaimani kabisa mtaenda kutoa taarifa sahihi kuhusu mradi. Nawasihi mtumie kalamu, kamera zenu vizuri kuhabarisha jamii.

Serikali inaendelea kutekeleza mradi huu mkubwa kwa manufaa ya Watanzania hivyo ni vyema Watanzania wakaufahamu mradi huu”, ameongeza Mhe. Samizi.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu amesema wananchi ambao maeneo yao yamepitiwa na mradi asilimia kubwa wamelipwa fidia ikiwemo kujengewa nyumba za kisasa, huku wakandarasi wazawa wakipata kazi katika mradi huo.

Mratibu wa Mradi wa EACOP kitaifa, Asiadi Mrutu amesema
Urefu wa Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga Nchini Tanzania ni 1,443 km/Inchi 24 ambapo Uganda ni 296km na Tanzania 1,147km.


"Gharama za mradi USD 5.088 Bilioni utakuwa na uwezo wa kupitisha mapipa 216,000/ kwa siku. Muda wa Ujenzi wa Bomba ni Miezi 24 kuanzia Januari 2024 ambapo Mikoa inayopitiwa na Bomba kwa Tanzania ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga",ameeleza.


Mrutu amezitaja shughuli zinazoendelea kwa upande wa Tanzania kuwa ni Utwaaji wa ardhi ya mkuza wa bomba (Kagera mpaka Tanga), Kazi za awali za ujenzi wa makambi (Kambi Na. 6,7,8,9,10,11,15), Ujenzi wa karakana ya kuandaa mabomba – Sojo-Nzega, Ujenzi wa kituo cha Bandari – Chongoleani, Manunuzi ya wakandarasi, watoa huduma na ajira, miradi ya maji na umeme na ujenzi wa nyumba za wananchi waliopisha maeneo ya mradi.


"Mradi unatekeleza zoezi la uelimishaji na ulipaji fidia kwamujibu wa Sheria za Tanzania na taratibu za kimataifa (IFC). Mpaka tarehe 21 Septemba 2023 jumla ya wananchi 9,815kati ya 9,898 wamesaini mikataba ya fidia na kati yao wananchi 9,813 wamelipwa fidia TZS34.89Bilioni sawa na 99.1%; na Wananchi 83 waliobakia wanaendelea kukamilisha taratibu iliwaweze kusaini mikataba ya fidia na kupokea stahiki zao",ameongeza.


Akizungumzia kuhusu ujenzi wa Karakana ya Sojo Nzega Tabora, Mrutu amesema ujenzi wa jengo la karakana umekamilika kwa 100%, jumla ya Watanzania 426 wamepata ajira sawa na 95% na kwamba Kampuni 20 za Kitanzania zimetoa huduma zenye thamani ya TZS47bilioni.

"Ufungaji wa mitambo ya karakana unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba 2023 na tayari vipande 20 vya mabomba vimewasili kwa ajili ya majaribio ya karakana",amesema.

Mrutu amesema Utekelezaji wa mradi unaendelea vizuri (25% kwa ujumla), zoezi la ulipaji fidia linaendelea vizuri (99% kwa ujumla) na kwamba Serikali inaendelea kushirikiana na EACOP kutoa elimu kwajamii kitaifa na kimataifa.


Nao waandishi wa habari waliopata mafunzo hayo wamesema yamewasaidia kujua kuhusu maendeleo ya mradi huo na faida kwa jamii yote inayopitiwa na mradi pamoja na nchi kwa ujumla.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mafunzo yakiendelea
Afisa Uhusiano TPDC, Francis Lupokela akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Afisa Uhusiano TPDC, Francis Lupokela  akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano EACOP, Catherine Mbatia  akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano EACOP, Catherine Mbatia  akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Afisa Habari EACOP, Abbas Abraham akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Afisa Habari EACOP, Abbas Abraham akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Afisa Fursa kwa Wazawa EACOP, Maryam Mandia akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP
Mratibu wa Mahusiano ya jamii EACOP Shinyanga, Cecilia Nzeganije akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Mradi wa EACOP


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA