Na Mwandishi Wetu, IRINGA
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Bernard Marcelline ameipongeza timu ya wanawake ya Wizara hiyo kwa kuibuka mshindi kwenye mchezo wa kamba waliocheza dhidi ya Tume ya Sheria ETC.
Akizungumza leo kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayofanyika mkoani Iringa, Bw. Marcelline amesema kwa wale ambao walipoteza michezo mingine bado wanayo nafasi ya kujipanga zaidi ili hatimaye kupata ushindi.
"Tuna imani kubwa mtafanya vizuri zaidi na kwa niaba ya Menejimenti ya Wizara nimekuja kuwaambia kuwa wapo na ninyi katika kila hatua", amesema.
Aidha, amesema michezo hiyo ina malengo mbalimbali ikiwemo kujenga mahusiano ya kikazi kati ya taasisi zao na watu wanaocheza nao.
"Kwa hiyo ushindi wa kwanza ni kwamba mmeshiriki, Ushindi wa pili mnajenga mahusiano na taasisi nyingine", ameongeza.
Wakati huo huo, amesema Wizara inatambua juhudi hizo na kujitolea kwao.
"Tunatambua kwamba mtapata vikombe. Nitakuwa nanyi kesho wakati wa mechi nikiwatia moyo lengo letu hapa ni ushindi, Tushangilie vizuri, tuhakikishe hii kamba inakatika",amesema.
Post a Comment