MHE. KAIRUKI ATAJA TAREHE ZA ONESHO LA SITE 2024


Na John Mapepele

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ametangaza  tarehe  ya maonesho ya nane ya Swahili International Tourism Expo - S!TE, 2024 kuwa ni  Oktoba 11-13 na  kuwataka waandaaji kuyaboresha zaidi ili kupata washiriki wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Mhe. Kairuki ametoa kauli hiyo leo Oktoba 8,2023 katika siku ya mwisho ya Maonesho ya Saba ya Swahili International Tourism Expo- S!TE 2023 wakati  akifunga maonesho  hayo  jijini Dar es Salaam.


Amewashukuru wadau wote walioshiriki kwenye maonesho ya mwaka huu ambapo amesema   bila ushiriki wao lisingeweza kufanyika kwa kiwango na ubora   mkubwa  kama lilivyofanyika.


Ameipongeza Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kupamba maonesho hayo kwa kuandaa bustani ya wanyamapori hai ambayo imekuwa kivutio kikubwa kwa watu waliotembelea.


Aidha amewaomba wadau  kutoa maoni  kuhusu maonesho ya mwaka huu  ili yasaidie  kuboresha  maonesho  ya mwakani na  kuyafanya  kuwa ya  kimataifa.


“Maboresho  haya yatatujenga  na kutusaidia   kutuingiza katika  maonesho  makubwa  ya kimataifa  kama  vile world tourism Market.” amefafanua  Mhe. Kairuki


Awali Mhe. Kairuki alisema pamoja na kazi kubwa ya kuboresha miundombinu iliyofanywa na kusaidia kuleta watalii pia alifafanua kuwa ongezeko  kubwa la watalii nchini limetokana na kazi nzuri iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya “The Royal Tour”. Filamu hii ilionyeshwa katika vituo vingi vya televisheni vinavyotambulika nchini Marekani na kwingineko duniani ili kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania.









Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA