MRADI WA UMEME WA IJANGALA WA KW 360 KUUNGANISHWA KATIKA GRIDI YA TAIFA, NJOMBE KUNUFAIKA


Mradi wa Umeme wa Ijangala utakaozalisha Kilowati 360 umekamilika na unatarajiwa kuzinduliwa hivi Karibuni.


Mradi huo utakaoungwa kwenye Gridi ya Taifa, utaimarisha hali ya upatikanaji umeme kwa wakazi wa Njombe na kuimarisha uendelezaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi.


Ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uzinduzi wa Mradi huo, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu  Mha. Innocent  Luoga  wa Wizara ya Nishati tarehe 25 Oktoba, 2023 ametembelea  na kukagua mradi huo wa Umeme wa Ijangala uliopo Kijiji cha Masisiwe Wilaya ya Makete Mkoani Njombe ili kujionea maandalizi ya uzinduzi wa mradi huo na ameelezea kuridhishwa kwake na hali ya maandalizi.

Mha. Innocent  Luoga amesema kuwa, Mradi huo unaomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kusini kati una Mitambo mitatu ya uzalishaji Umeme  inayofanya kazi vizuri na maji  yanapatikana ya kutosha katika eneo hilo.


Amebainisha kuwa  Umeme huo utaunganishwa katika Gridi ya Taifa na hivyo kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kijamii na kiuchumi.


Aidha Kamishna Luoga amemshukuru Baba Askofu Wilson Sanga ambae ni Mkuu wa Dayosisi ya Kusini Kati kwa kubuni mradi huo ambao utaongeza uzalishaji wa umeme nchini na kuahidi kuwa Wizara ya Nishati itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kuhusiana na mradi huo.


"Serikali inaendelea kutoa wito Kwa Taasisi binafsi na za kidini kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kubuni na kuendeleza Miradi ya uzalishaji Umeme kwa kupitia Taasisi zetu za Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ili kuhakikisha

 nchi yetu inakuwa na umeme wa kutosha, wa uhakika na wa bei nafuu." Amesema Mha. Luoga

 

Katika ziara hiyo  Kamishna Luoga ameongozana na Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati, REA na TANESCO akiwemo Mkurugenzi wa TANESCO Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mha.Sotco Nombo.



Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA