Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, tarehe 3 Oktoba, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Ghana Mhe. Alban Bagbin katika ofisi za Spika wa Ghana zilizopo Jijini Accra.
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amemueleza Spika huyo kuhusu nia yake ya kugombea nafasi ya Urais wa Umoja wa Mabunge duniani (IPU) katika uchuguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Ockoba 2023 Luanda nchini Angola ambapo Mhe. Bagbin amemtakia kila la kheri kwenye uchaguzi huo.
Post a Comment