WAFANYAKAZI WA WIZARA YA MADINI WATEMBELEA MIGODI YA BARRICK BULYANHULU NA NORTH MARA NA KUVUTIWA NA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA ZA KISASA

 

Mhandisi wa Madini Mwandamizi katika mgodi wa Bulyanhulu,Innocent Matembe, akiwaeleza watumishi wa Wizara ya Madini mchakato wa uzalishaji kwa kutumia teknolojia za kisasa.
Watumishi wa Wizara ya Madini wakipata maelezo kutoka vitengo mbalimbali vya uzalishaji katika mgodi wa Bulyanhulu
Watumishi wa Wizara ya Madini wakipata maelezo kutoka vitengo mbalimbali vya uzalishaji katika mgodi wa Bulyanhulu
Watumishi wa Wizara ya madini wakipata maelezo ya utendaji kazi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu katika kikao cha pamoja na wafanyakazi kutoka Wizara ya Madini.
Watumishi wa Wizara ya madini wakiwa katika eneo la mgodi wa chini ya ardhi North Mara.
Watumishi wa Wizara ya madini wakiangalia moja ya mradi uliotekelezwa na mgodi wa Barrick North Mara katika eneo la Nyangoto.


Watumishi wapatao 14 kutoka kada mbalimbali za Wizara ya Madini ikihusisha Makatibu Mahususi, Watunza Kumbukumbu na Wahudumu wametembelea migodi wa Barrick North Mara na Barrick Bulyanhulu iliyopo katika mikoa ya Shinyanga na Mara na kuvutiwa na matumizi ya teknolojia za kisasa katika uchimbaji wa madini zinazotumika katika migodi hiyo .

Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa kutembelea migodi katika utekelezaji wa maazimio ya Wizara ya Madini wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo lililofanyika mwezi Mei, 2023, jijini Dodoma ambapo kundi la kwanza lilitembelea migodi mwezi Agosti mwaka huu.



Aidha, ziara hiyo inalenga kuwajengea uelewa wa pamoja watumishi wote wa Wizara kuhusu shughuli zinazofanywa katika Sekta ya Madini hususan shughuli za uchimbaji wa madini katika migodi mikubwa, ya kati na midogo ili kuwezesha malengo mahususi ya wizara kutekelezwa kwa pamoja kama familia moja ya Madini.



Watumishi hao wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali katika migodi hiyo ikiwemo mgodi wa chini (Underground Mining), sehemu ya uchenjuaji (Processing Plant) bwawa la huifadhi tope sumu ( TSF) , sehemu ya upokeaji na utunzanji wa vifaa vinavyotumika katika migodi pamoja na kutembelea miradi ya jamii inayotekelezwa na migodi hiyo kupitia Mpango wa Uwajibikaji wa Migodi kwa Jamii (CSR).


Hili ni kundi la pili la watumishi wa kada hizo kutembelea maeneo ya migodi ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa.


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA