Mratibu wa Taasisi ya Uringo Dkt. Ave - Maria Semakafu akitoa mada kuhusu Madai ya Mabadiliko kwenye Katiba na Mtandao wa Wanawake na Katiba
Mratibu wa Taasisi ya Uringo Dkt. Ave - Maria Semakafu akitoa mada kuhusu Madai ya Mabadiliko kwenye Katiba na Mtandao wa Wanawake na Katiba
Na Holiness Ulomi - Dar es salaam
Katika siku ya pili ya Tamasha la 15 la jinsia leo Jumatano Novemba 8,2023 katika viwanja vya mtandao na jinsia Tanzania TGNP jijini Dar es salaam, Mratibu wa Taasisi ya Uringo Dkt. Ave - Maria Semakafu ametoa hoja mbalimbali juu ya mabadiliko kwenye katiba.
Dkt. Ave Maria ametoa Hoja wakati akitoa mada kuhusu Mabadiliko kwenye Katiba na Mtandao wa Wanawake na Katiba wakati wa Warsha ya Ujenzi wa Harakati katika kuhamasisha uongozi kwa wanawake, kukuza sauti zao na Ushiriki katika siasa na nafasi za uongozi
Amesema kuendeleza mfumo wa Viti Maalum kwa wanawake unaathiri wanawake kwani umejaa ubaguzi na udhalilishaji wa Kijinsia kama itawezekana basi mfumo huo ubadilishwe au kuondolewa kabisa.
Mbali na hayo Dkt. Ave- Maria amegusia namna tunavyohitaji Tunahi usawa nusu kwa nusu na pia wanawake wengi wajitokeze kushika nafasi za uongozi na ngazi za maamuzi. Kwa upande wa ushiriki wa wanawake kwenye siasa, waleteni wanawake tuje tuwapigie kura badala ya kuchaguliwa na chama cha siasa kwani hii itasaidia kwenye kuhakikisha hali ya usawa katika Jamii.
Post a Comment