Kufuatia Shilingi 3.6 Billioni zilizotolewa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vituo 16 vya afya nchini, kituo Cha afya Chibumagwa ni miongoni mwa vituo vilivyopewa vifaa vyote vya vya upasuaji na watoto njiti Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo Novemba 17, 2023 kutoka Idara ya Bohari ya Madawa MSD (Medical Store Department.) Mbunge wa Manyoni Mashariki Mheshimiwa Dkt. Pius Chaya ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia kwa vifaa hivyo ambavyo vitasaidia kutoa huduma bora ya mama na mtoto.
"Mheshimiwa Rais ametoa 3.6bn kwa vituo 16 Tanzania nzima ambapo Chibumagwa ni kati ya vituo ambavyo vinapewa vifaa vyote vya upasuaji, Kituo Cha Chibumagwa kitakuwa cha mfano kwa Manyoni kwa kutoa huduma bora ya Mama na Mtoto" Amesema Mbunge Dkt. Chaya
Pamoja na mambo mengine Mbunge huyo ametoa wito wa kufanyika utaratibu wa kufungua kituo rasmi na vifaa kufanyika haraka iwezekanavyo.
"Tunashauri utaratibu wa kutoa hamasa kupitia kufungua kituo rasmi na vifaa ufanyike haraka" Amesema Dkt. Chaya.
Ikumbukwe kuwa katika Billioni 3.6 iliyotolewa kwa vituo 16 nchini, kwa kituo Cha afya Chibumagwa kimepokea vifaa vyenye thamani ya shilingi 175 Milioni kwa Kanda ya Kati.
Post a Comment