MICHEZO YA 13 YA MABUNGE YA AFRIKA MASHARIKI YAENDELEA


Michezo ya 13 ya Mabunge ya Afrika Mashariki imeendelea tena leo Jumanne hapa Kigali ambapo katika mchezo wa Kikapu Wanaume Bunge SC imefungwa na Uganda kwa Vikapu 37-32, wakati dada zao wakawalipia kisasi kwa kuwachapa Wabunge wa Uganda kwa Vikapu 31-27.
Mchezo wa Darts kwa upande wa Wanaume Tanzania iliwasilishwa na Yahya Masare  ilipoteza kwa 2-0 lakini Masare akasahihisha makosa na  kuwachapa Bunge la Afrka Mashariki kwa 2-0

Mchezaji mwingine Kwa upande wa wanaume Yahya Mhata alipoteza kwa 0-2 dhidi ya Uganda, lakini na yeye akalipa kisasi kwa Sudani Kusini kwa Ushindi wa 2-0.

Kesho jumatano Bunge SC-Soka maarufu kama Tulia Boys ambayo imejizolea umaarufu kutokana na soka la kuvutia itavaana na Wenyeji Rwanda. 

Taarifa na Cosato Chumi Gaza Mbunge wa Mafinga Mjini na Captain wa Bunge SC -Soka.


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA