MBUNGE APAZA SAUTI SUALA LA BIMA, SERIKALI KUANZA KUWAJENGEA UELEWA WANANCHI NA WADAU KUHUSU BIMA YA TANZANIA


                 Na, Mwandishi Wetu - Dodoma.

Kufuatia swali la Msingi la Mbuge wa Muleba Kusini Mheshimiwa Dkt. Dkt. Oscar Kikoyo  alilouliza leo tarehe 31 januari 2024 bungeni kuwa "Je, ni lini Serikali itarekebisha Sheria ya Bima ya Tanzania kwa lengo la kuweka kima cha chini cha malipo ya fidia kwa wahanga wa ajali za barabarani?."


Serikali itaendelea na jitihada za kujenga uelewa kwa wadau wa tasnia ya bima na wananchi kwa ujumla ili kutimiza matakwa ya Sheria ya Bima, Sura 394 ikiwemo kuboresha huduma za bima na kumlinda mteja.

Majibu hayo ya serikali yametolewa na Waziri wa Fedha Mhe. dkt. Mwigulu Nchembawakati akijibu swali hilo la msingi ambapo amesema kuwa mnamo Septemba 2022 Mamlaka ya Bima Tanzania ilitoa Mwongozo unaotambulika kama “Mwongozo wa Viwango Elekezi vya Fidia ya Bima kwa Madai ya Majeraha ya Mwili na Vifo kwa Mtu wa Tatu Kutokana na Ajali za Vyombo vya Moto”. Mwongozo huo ulitolewa kwa mujibu wa Kifungu cha 6(2) (e) na 11 (a) na (b) cha Sheria ya Bima Sura Na. 394. Aidha, lengo la Mwongozo huo ni kuweka usawa na ubora katika ulipaji wa fidia zitokanazo na madai ya bima.
 
MATUKIO MBALIMBALI WAKATI BUNGE LIKIPITISHA MPANGO WA TAIFA WA MAENDELEO YA  MIAKA MITANO, BUNGENI DODOMA - HABARI MSETO BLOG

"Utekelezaji wa mwongozo huo umepunguza kwa sehemu kubwa malalamiko kutoka kwa wahanga wa ajali za vyombo vya moto kwa kuwa kuna usawa katika suala la viwango vya fidia vinavyotolewa na kampuni za bima. Pamoja na mafanikio yaliyopatikana, napenda kutumia fursa hii kuwaasa wananchi kutunza kumbukumbu na nyaraka muhimu za rejea ili kurahisisha zoezi la ulipaji wa fidia, hususan kwa wasimamizi wa mirathi." 

Kwa majibu hayo yakamfanya mbunge huyo kuongeza swali la nyongeza kwa muktadha wa kujua "Tatizo la kudai bima limekuwa sugu ningependa kujua ni nani anasimamia kikamilifu huo mwongozo.?" ndipo Dkt. Nchemba akatolea ufafanuzi na kutoa wito kwa wananchi kutunza kumbu kumbu.
 
"Nitoe wito kwa wananchi kutunza kumbukumbu muhimu za nyaraka rejea ili kurahisisha zoezi la ulipaji wa fidia hususani kwa wasimamizi wa mirathi." Amesema Dkt. Nchemba
 


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA