WANA KAGERA KWENDA KIZIMKAZI ZANZIBAR KUMPONGEZA RAIS SAMIA KUIFUNGUA KAGERA

   

Mwenyekiti wa taasisi ya Mtetezi wa Mama mkoa Kagera ndg Kauthari Chamani akizungumza baada ya kukabidhi mchango wa kufanikisha safari ya Zanzibar kwa mratibu mkuu wa safari hiyo Enock Bujuli.
Mwenyekiti wa taasisi ya Mtetezi wa Mama mkoa Kagera ndg Kauthari Chamani (kushoto) akikabidhi mchango wa kufanikisha safari ya Zanzibar kwa mratibu mkuu wa safari hiyo Enock Bujuli.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Wananchi wa Mkoa wa Kagera kupitia kikundi cha wakulima wa zao la Kahawa maarufu Smart Coffee Day Tours wamepanga safari ya kwenda  Kizimkazi Zanzibar kwa ajili ya kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuifungua Kagera kupitia zao la  Kahawa.

Akizungumza na Malunde 1 blog Mratibu Mkuu wa Safari ya Wana Kagera kwenda Kizimkazi Zanzibar , Enock Bujuli amesema sababu kuu za safari hiyo ndefu kwenda kumshukuru Mhe. Rais Samia ni kuonesha thamani ya zawadi inayotokana na upendo wa Rais Samia kwa wakulima wa zai la kahawa kwa kuweka mnada wa wazi Bukoba ambapo mkulima anapata pesa yake yote tena bei kubwa tangu nchi ipate Uhuru lakini pia kuwashukuru watu waliomlea Rais Samia kwa malezi mazuri na ya maadili mema.

"Tumeandaa zawadi maalum kwa ajili ya Rais Samia. Tayari wadau wanaendelea kutoa michango yao ili kufanikisha safari hii ya kihistoria itakayofanyika Mwezi Februari 2024 ambayo pia itabeba vikundi vya ngoma maalum zenye ujumbe, viongozi wa dini. Leo Januari 30,2024 Mwenyekiti wa taasisi ya Mtetezi wa Mama mkoa wa Kagera Kauthari Chamani, amekabidhi mchango wake kwa mratibu wa safari hii muhimu Enock Bujuli",amesema Bujuli.


Amefafanua kuwa, kupitia kumpongeza Dkt. Samia Suluhu Hassan  wanataka dunia ijue kazi nzuri inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wana Kagera na katika maandalizi ya safari hiyo ya kihistoria wameanza kupokea michango ili kuwezesha makundi yenye ujumbe wa zawadi, nyimbo na viongozi wa dini kusafiri kutoka Kagera kwenda Zanzibar.

"Kwa yeyote anayewiwa kutuchangia katika safari yetu ya kutoka Kagera kwenda Kizimkazi Zanzibar awasilishe mchango wake kupitia Akaunti ya SMART COFEE DAY TOURS akaunti namba 0133839710100, Benki ya CRDB au kwa Enock Bujuli (Mratibu) - 0717361886 au Justinian Kazunguru (Mwenyekiti wa Wazee) - 0759453916 au Kokuirwa Bagwerwa (Mshauri mkuu) - 0784467175",ameongeza Bujuli.

"Kikundi chetu cha Smart Coffee Day Tours,tumesajiliwa wilaya Karagwe lakini wanachama wanatokea wilaya zote za Mkoa Kagera. Kazi yetu kubwa ni kuitangazia dunia uzuri wa zao la kahawa pia kusherekea kwa kuwapongeza wote wenye mchango mkubwa katika zao la kahawa na kwa mara ya kwanza tunaanza na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameruhusu ushindani katika kununua za la kahawa lakini tofauti na miaka mingine ambapo bei ya kahawa ilipangwa na kundi dogo la watu na hata iliponunuliwa malipo yalitoka kidogo kidogo. Hili ni jambo kubwa sana lazima tumpongeza Rais wetu mpendwa",ameeleza Bujuli.
Mzee mshauri Justinian Kazunguru akimshukuru Mwenyekiti wa taasisi ya Mtetezi wa Mama mkoa Kagera ndg Kauthari Chamani kwa kukabidhi mchango wa kufanikisha safari ya Zanzibar 
Picha ya pamoja
Kikao cha kamati kikiendelea, kushoto ni Mzee Richard Byanjweri kutoka Kyerwa akisikiliza mratibu mkuu wa safari hiyo Enock Bujuli akitoa ufafanuzi juu ya maandalizi  ya safari ya Wana Kagera kutoka Kagera kwenda Zanzibar
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA