Na Angela Msimbira OR -TAMISEMI
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Dkt.Festo Dugange amesema inalipa kwa wakati posho kwa madiwani na hakuna diwani anayekopwa.
Dk Dugange ametoa kauli hiyo akujibu hoja zilizotolewa na wabunge wakati wa kuchangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2023.
Amesema kuwa Serikali inatumbua kazi kubwa inayofanywa na madiwani na wenyeviti wa vijiji ndio maana katika mwaka wa fedha 2021/22 ilianzisha kulipa posho kwa madiwani katika halmashauri 128
"Kipindi cha nyuma madiwani walikuwa wakikopwa fedha zao lakini hivi sasa Serikali inalipa posho za madiwani kwa halmashauri 168 na hakuna diwani anayekopwa posho yake,"amesma Dkt. Dugange
Amesema Serikali inafahamu unahitajika wa kuongeza kiwango cha posho, lakini kwa sasa serikali inaendela kuongeza uwezo wa kukusanya wapato ili kuweza kufanyiakazi suala la posho za madiwani na wenyeviti wa mitaa
Kuhusu hoja ya posho za watendaji wa kata, Dk Dugange alisema maelekezo ya Serikali kwa wakurugenzi wa halmashauri ni kulipa posho na watendaji wa kata kwa wakati.
"Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita halmashauri 80 kati ya 184 ambazo hazikulipa posho hizi, serikali imechukua hatua kwa kuhakikisha wanalipa posho kwa wakati na kundelea kutenga fedha kwa ajili ya posho hizo."
Aidha, Dk Dugange amewaagiza viongozi wote kuhakikisha wanatatua kero za wananchi kwa wakati na si kuziacha mpaka viongozi wakubwa waje kushughulikia kero hizo
"Kero nyingi zinaweza kutatuliwa na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi, tofauti na hapo serikali haitosita kutengua uteuzi wao."
Post a Comment