Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Uchukuzi wa Misri L.G, Kamel Alwazeer na ujumbe alioambatana nao na kujadili masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Misri katika Sekta Ujenzi.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 20 Februari, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Dar es salaaam (JNICC).
Kikao hicho kimeshirikisha Viongozi na wataalam kutoka Wizara ya Ujenzi, ikiwa ni pamoja Wakurugenzi kutoka Wizara ya Ujenzi, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Post a Comment