MATIKO ASHIRIKI VIKAO VYA MKUTANO WA UMOJA WA MABUNGE DUNIANI (IPU)


Pichani ni Mhe Esther Nicholas Matiko akishiriki mwendelezo wa vikao vya Mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) vinavyoendelea Geneva nchini Uswisi.


Kikao hicho kimejadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kujumuisha mambo ya dharula kwenye mkutano huo, majadiliano ya mandhari ya demokrasia za kibunge, ujenzi wa daraja baina ya Amani na ufahamu, umuhimu wa uwajibikaji na utekelezaji wa maazimio ya IPU na maamuzi mengine, uwasilishwaji wa matokeo ya matumizi ya mfumo wa silaha za kujitawala na akili bandia.


Vile vile kikao hicho ikiwa ni sehemu ya mkutano wa 148 wa IPU umejadili kuhusu uhusiano wa matokeo ya hali ya hewa, kuwezesha ufikiwaji na upatikanaji wa nishati ya kijani na uhakikishwaji wa ubunifu na usawa, taarifa za kamati za kudumu za IPU na kupitisha vifungu vya kamati ya kudumu ya Amani na Usalama wa Kimataifa na kamati ya kudumu ya Maendeleo Endelevu kwa ajili ya mkutano wa 150 wa IPU.




Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA