Mbio za Mwenge wa uhuru zinatarajiwa kuzinduliwa Mkoani Kilimanjaro mnamo Aprili 2, 2024 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Ikumbukwe kuwa kwa mara ya kwanza Mwenge huo uliwashwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro mnamo Desemba 9, 1961 ukiashiria kuangaza nchi na kuvuka mipaka kuleta matumaini palipo kukata tamaa, upendo pale kwenye chuki na heshima pale kwenye dharau.
Kila mwaka mbio hizi huanzia katika mikoa tofauti tofauti hapa Nchini yenye lengo la kuwakumbusha Watanzania kuwa ni jukumu lao la Kulinda umoja na amani ya nchi.
Aidha mbio hizo huenda sambamba na ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Mkoa husika ambayo imekwisha tekelezwa na inayoendelea kutekelezwa.
Hata hivyo Uzinduzi huo Mkoani humo utaenda sambamba na kauli Mbiu "Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu"
Post a Comment