Mfahamu Thomas Fuller "Negro Demus" mwafrika aliyesafirishwa na kwenda kuwa mtumwa Marekani mnamo 1724. Huyu bwana alikuwa mahiri sana kwenye kufanya mahesabu, hakika alikuwa na uwezo wa ajabu. (1710-Disemba1790)
Kipawa chake kilionekana na watu ambao walikuwa wakipinga biashara ya utumwa, na walimchukua ikawa wanatembea nae kama mfano kuwa watu weusi wenye akili kuliko wazungu wapo, hivyo sio kweli kuwa wazungu mara zote ni werevu kuliko watu weusi.
Asili ya nchi aliyotoka bado ni tata, ila inaaminika ni kati ya nchi ya Liberia au Benin. Walimfupisha wakamuita ‘Negro Tom’, na aliishi Virginia kama mtumwa tangu alipotwekwa kwao na kuuzwa Marekani akiwa na umri wa miaka 14 tu. Na huko Virginia, walimtambua kama ‘Virginia Calculator’.
Bwana Tom alipokua na umri wa miaka 70, watu wawili raia wa Pennsylvania Bw. William Hartshorne na Samuel Coartes walisikia habari za bwana Tom, uwezo wake katika hesabu aliokua nao. Mabwana hawa walikwenda na maswali yao waliamini yatakuwa magumu kwa Tom, ila walijua kuwa hawajua walipokutana na Tom.
Swali la kwanza walimuuliza bwana Tom kuwa kuna sekunde ngapi ndani ya mwaka mmoja na nusu? Tom alitumia dakika mbili tu kutoa jibu sahihi (47,304,000)... Jamaa wale wakameza mate wakaona hapa kweli kazi ipo, wakauliza swali la pili, “Binadamu aliyeishi miaka 70, siku 17 na masaa 12, jumla itakuwa ameishi sekunde ngapi”? Bw. Tom alitumia dakika moja na nusu tu kujibu swali hilo, yani lilikuwa jepesi sana kuliko la kwanza, Tom akatoa jibu kwamba ni sekunde 2,210,500,800.
Tom alipotoa hilo jibu, kulikuwa na jamaa pembeni ana kalamu na karatasi kuhakiki majibu ya Tom, mara jamaa akasikika akisema kuwa Tom amekosa, kuwa Tom ametaja namba kubwa zaidi na sio jibu sahihi. Tom akatabasamu tu, halafu mmoja wa wale jamaa akauliza jamani mmehesabu sekunde za “leap year”?.... Walipohesabu sekunde za siku za “Leap Year”, majibu yakaja sawa kabisa kama alivyosema Tom.
‘Leap year’, ni mwaka ambao mwezi wake wa Februari unakua na siku 29 badala ya 28, na mwezi huu huja kila baada ya miaka minne. Sasa hawa mabwana walisahau wakawa wamezidisha miezi ya februari ya siku 28 tu, kumbe kuna siku kibao kwenye februari zenye siku 29 ambazo sekunde zake hawakuzihesabu. Wakapiga tena hesabu, Tom akawa sahihi.
Inasemekana kuwa huyu Mwamba alifariki akiwa na umri wa miaka 80, akiwa hajui kusoma wala kuandika jina lake. Huyo ndio Tom.
Post a Comment