Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka ameshambuliwa kwa risasi na watu wasiojuikana katika eneo la Wilaya ya Kiteto majira ya saa moja kasoro usiku wa kuamkia Jumamosi Machi 30, 2024
Akihojiwa kwa njia ya simu na moja ya Chombo Cha habari hapa nchini amethibitisha taarifa hiyo iliyokuwa inasambaa kwenye mitandao ya kijami.
Akielezea tukio hilo amesema "Kuna gari iliyokuwa inatufuatilia kwa nyuma tukaipisha kidogo kwa upande wa kulia walivyofikia usawa wetu wakaanza kumimina risasi kwa dereva na baada ya hapo wakavuta kwenda mbele wakaanza kupiga za usoni na sisi tukakata kona kugeuza na mimi nikapigapiga za juu pale kuwatishia tishia ndipo tukafanikiwa kugeuza na kuondoka" Amesema Olesendeka
"Walikuwa wana silaha kubwa na ndogo, mpaka sasa hakuna aliyepata madhara ni gari tu wamelichakaza kwa sababu bado tuko gizani sijajua ni ngapi ila kwa haraka haraka ni nne za waziwazi, bado siwezi kusema jambo kwa wakati huu" Olesendeka.
Baada ya tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Lucas Mwakatundu akadhibitisha jeshi la polisi kupokea taarifa ya tukio hilo.
Post a Comment