Kufuatia taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani Manyara ya kumshikilia Edward Erihard (31), mkazi wa Mkoa wa Dodoma akituhumiwa kusafirisha wahamiaji haramu 20 raia wa Ethiopia kwa kutumia gari aina ya toyota Land Cruiser V8, Gari lililodaiwa kuwa lilikuwa linapeperusha bendera ya CCM, lengo lilikuwa kuonyesha kuna kiongozi wa chama hicho anasafiri.
Licha ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara, John Nzwalile kulaani kitendo hicho kumeibua mijadala mbalimbali ya wananchi wakitoa maoni kuwa "Sisi wananchi siku nyingi sana tunajua ukiona gari inapeperusha bendera ya CCM ( bendera ya nje au bendera ya kuning'iniza ndani ya gari) inajambo la magendo inasafirisha au Kuna uvunjifu wa sheria wanafanya, Ila tulikuwa tunajua wanafanya hivyo kwa sababu ya urafiki na uswahiba wa CCM na vyombo vyake vya Dola, hivyo wao CCM wanaruhusiwa kuvunja sheria?"
Maoni Mengine yaliyoibua hisia za wengi na maswali ni;
-Magari yenye bendera za CCM hayafuati na kuheshimu sheria za Usalama barabarani 100%?
-Magari yenye bendera kwenye sehemu za kuendesha speed 50,wao wanaendesha speed 180 na hakuna kitu wanafamywa?
-Magari yenye bendera za CCM hayakaguliwi ndani yamebeba nini hata katika vizuizi vya barabarani kama magari ya Raia wengine?
-Magari yenye bendera za CCM hayakaguliwi vitu muhimu kama bima ya gari kama ipo au haipo.?
-Magari yenye bendera za CCM hayahitaji stika za usalama wa nenda kwa usalama, stika yake ni bendera ya CCM.?
Post a Comment