SERIKALI YATATUA MGOGORO WA MUDA MREFU KATIKA MGODI WA MALERA - TARIME MKOANI MARA

 

Na Ernest makanya,Mara 


WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde kwa kushirikiana na Mkuu Wa Mkoa Wa Mara Said Mtanda  wametatua  mgogoro baina ya wachimbaji wadogo na  wamiliki wa leseni na Kampuni ya KIRIBO katika mgodi wa Malera ambako kulikuwa na zuio la mgao wa mawe ya dhahabu.


Waziri Mavunde alitumia saa kadhaa kutatua mgogoro huo mgodini hapo jana Jumatatu, kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara Said Mtanda na watendaji wa wizara na viongozi wa wachimbaji wadogo wa mgodi wa  (MAREMA).


Waziri huyo mwenye dhamana ya madini alizipongeza pande zote kwa kuridhia makubaliano katika hatua ya awali ya kutatua mgogoro huo


“Ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan juu ya utatuzi wa migogoro mbalimbali katika sekta hii ya madini, ambayo inadhoofisha kukua kwa uzalishaji wa madini,” alisema Mavunde.


Waziri Mavunde Alielekeza zuio la mgao wa mawe ya dhahabu yaliyozalishwa mgodini hapo liondolewe na mgao wa mawe uanze mapema leo Jumanne.


"Pia hakikisheni katika utekelezaji wa maridhiano haya, wachimbaji wadogo hawaondolewi katika eneo hilo na waachwe waendelee na shughuli zao,” aliagiza Waziri Mavunde.


Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mohamed Mtanda alimshukuru Waziri Mavunde kwa kufanikisha utatuzi wa mgogoro huo kwa kuruhusu mgao wa mawe uendelee kwani kipato cha wananchi wa eneo hilo kilikuwa kimeshuka na mapato ya serikali yalikuwa hayapatikani kwa wakati.


Watu zaidi ya 2,000 wananufaika na mgodi huo wa Malera uliopo wilayani Tarime, Mara ambao umekuwa ni shughuli kubwa ya kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA