Katika kuadhimisha siku hiyo Wanawake wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wameshiriki maadhimisho hayo yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mjini Mwema wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam ikiwa kauli mbiu ya mwaka huu ni "Wekeza kwa Mwanamke kuharakisha maendeleo ya taifa na ustawi wa Jamii".
Tarehe 8 Machi ya kila mwaka ni Siku ya wanawake duniani, ambapo siku hii inataka kukumbushia na kutafakari juu ya matokeo ya kisiasa, kijamii, kiuchumi waliyofikia wanawake na msimamo wao imara katika ngazi ya kijamii kwa ujumla.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa Wanawake TUGHE Tawi la TCAA Bi. Lydia Moffat amesema nguvu ya wanawake katika taasisi na mapambano ya kiuchumi inaonekana kwa uwazi na kutoa rai kwa wanawake wote waendelee kufanya kazi kwa bidii kila mmoja kwa nafasi yake kwani uwepo wake mahala hapo ni wa thamani sana.
Siku ya wanawake duniani ilianza kutokana na jitihada za wanawake 15,000 mwaka 1908 walipoandamana mjini New York Marekani wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura. Kilikuwa ni chama cha kisoshalisti cha Amerika kilichotangaza kuwa ni siku ya kwanza ya kitaifa ya wanawake, mwaka mmoja baadaye. Wazo la kuwa siku ya kimataifa lilianzishwa na mwanamke kwa jina la Clara Zetkin. Yeye alipendekeza wazo hilo mwaka 1910 katika mkutano wa kimataifa wa wafanyakazi wanawake huko Copenhagen Denmark.
Picha mbalimbali za matukio ya wafanyazi wanawake wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) katika maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo Machi 08, 2024 leo katika viwanja vya Mjini Mwema wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam ikiwa kauli mbiu ya mwaka huu ni "Wekeza kwa Mwanamkekuharakisha maendeleo ya taifa na ustawi wa Jamii"
Post a Comment