USWISI
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 22 Machi, 2024 ameshiriki vikao mbalimbali vikiwamo kikao cha Kamati ya Haki za Wabunge, Kundi la Mabunge ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Group), kikao cha Kundi la Kisiasa na Kijiografia cha Kanda ya Afrika (Africa Geopolitical Group), kikao cha Kundi la Kisiasa na Kijiografia la Twelve Plus na kikao cha ndani cha ngazi ya juu cha Usuluhishi wa Mgogoro wa Azerbaijan na Armenia.
Vikao hivi ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 148 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaotarajiwa kufunguliwa rasmi kesho 23 Machi, 2024 Geneva nchini Uswisi.
Post a Comment