*Falsafa ya 4R yampatia Rais Samia shahada nyingine ya udaktari
*Baada ya India, chuo kingine kikuu kikubwa cha Uturuki chamtunuku Rais Samia shahada ya udaktari
Aprili 18, 2024
Na Mwandishi Wetu - Zanzibar
Huku wakiwa wameshika bango lenye kauli mbiu maarufu ya "Songa na Samia," vijana wanaopiga mbizi kwa sarakasi kwenye eneo la Forodhani la Zanzibar, wametoa video yao mpya kuchambua falsafa ya 4R ya Rais Samia Suluhu Hassan kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Siku chache baada ya vijana hao kutoa video yao hiyo, Rais Samia ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi na Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki kwenye hafla iliyofanyika chuoni hapo Ankara, Uturuki, leo tarehe 18 Aprili, 2024.
Mwezi Oktoba mwaka jana, Rais Samia alitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa ya kielimu (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru nchini India. huku akiendelea na ziara yake nchini India.
Hadi sasa, Rais Samia ametunukiwa shahada za heshima takribani 4 kutoka vyuo vikuu vikubwa ndani ya nje ya nchi ndani ya miaka mitatu tu ya Urais wake.
Shahada hizo zinatambua jitihada kubwa inayofanywa na Serikali yake kuleta mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika sheria zetu za uchaguzi nchini.
Kwenye uongozi wake, Rais Samia anaamini katika kile kinachojulikana kama 4R – ikiwa ni ufupisho wa maneno manne ya lugha ya Kiingereza; Reconcilation (Maridhiano), Resilience (Ustahamiliivu), Reforms (Mabadiliko) na Rebuidlding (Kujanga Upya).
Hizi ndiyo 4R za Rais Samia ambazo zimeleta mafanikio makubwa kwenye uongozi wake tangu aingie madarakani Machi 19, 2021:
MARIDHIANO
Kwenye kujenga Tanzania bora,.Rais Samia amesema kuwa anatamani kujenga jamii yenye maridhiano na maelewano. Anatamani kujenga umoja pasipo kujali tofauti zetu za kisiasa, kidini, kikabila na nyingine zote.
Hili litawezekana kwa kujenga jamii inayopata haki sawa mbele ya sheria, isiyobaguana na inayotoa fursa sawa sawa za kiuchumi kwa wote.
Rais Samia anaamini kuwa maridhiano hayawezi kupatikana penye ubaguzi na pale ambapo kuna wanaokosa fursa na haki zao za kiuchumi na kiraia.
USTAHIMILIVU
Tanzania haiwezi kusonga mbele kama wananchi na viongozi watakuwa legelege kulinda yaliyo yetu. Wahenga walisema Umoja ni Nguvu na namna pekee ya kupambana na changamoto zote zinazoikumba dunia kwa sasa ni kwetu sisi kufanya hivyo kwa Umoja na Mshikamano.
Huko tuendako tutatikiswa na kuyumbishwa. Iwe kiuchumi, kimazingira, kijamii na kisiasa lakini ni lazima tujenge ustahamivu," Rais Samia alisema.
Hii ni kwa sababu hakuna nchi nyingine zaidi ya hii na hapa ndiyo kwetu. Nilitiwa nguvu sana na namna Watanzania walivyopokea tukio la Royal Tour kwa uzalendo wa kipekee.
MABADILIKO
Kuna msemo mmoja maarufu kwamba kitu pekee cha uhakika kwa mwanadamu ni mabadiliko.
Rais Samia amedhamiria kwamba serikali yake itajitahidi kufanya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika sheria zetu za uchaguzi.
Lengo ni kwamba Tanzania iende na wakati na – kama ilivyokuwa wakati mwingine, tujue mapema ni wakati gani wa kufanya jambo hata kama si watu wanaliunga au hawaliungi mkono kwa wakati husika.
Mabadiliko katika sheria za uchaguzi yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza. Kwenye uchumi, mabadiliko yatakuwa na lengo la kutoa fursa zaidi kwa watu wengi zaidi kunufaika kiuchumi badala ya wachache.
KUJENGA UPYA
"Ninafahamu kwamba wananchi hawali maridhiano, ustahamivu wala mabadiliko," Rais Samia alisema.
Kama walivyofanya watangulizi wa Rais Samia, lengo kuu linatakiwa kuwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Uchumi utakaoongeza ajira kwa vijana wetu na utakaofungua fursa kwa makundi yote ya kijamii yaliyo nchini.
Tayari serikali inaendeleza miradi mikubwa ya miundombinu na mengine kwenye sekta ya madini na nishati. Juhudi zilizofanywa kupitia kampeni ya Royal Tour zina lengo la kuzimua sekta muhimu ya utalii iliyoathiriwa sana na ugonjwa wa Covid 19. Katika kilimo serikali inafanya mabadiliko makubwa ili sekta hiyo muhimu ianze kuwa na mchango inaostahili kwenye uchumi wetu.
"Ninaamini kwamba kwa jitihada zetu za R nne, tutaweza kutimiza malengo ya kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa. Lengo kuu halikuwa kuwa na vyama vingi vya siasa bali lengo lilikuwa kujenga jamii yenye uzalendo, maridhiano, ustahamivu na yenye uchumi unaokua kwa wote na endelevu," Rais Samia alisema.
Post a Comment