Mtanzania anayejulikana kwa jina la Simon Mkondya ameanzisha kijiji cha Nguruwe katika kitongoji cha Zamahero kijiji cha Mayamaya wilayani Bahi mkoani Dodoma chenye nguruwe zaidi ya 800 na kuvutia maelfu ya watu kutoka ndani na nje ya Tanzania kutembelea kijiji hicho na kuona tamaduni zake.
Akizungumzia mradi huo alioubatiza jina Nguruwe Project mfugaji huyo amesema katika Kijiji hicho anafuga nguruwe wa aina tatu ikiwemo aina ya Large White ambao nyama yake imekuwa ikipendwa na wanawaķe kwa madai ya kwamba inasaidia kuongeza muonekano mzuri(shape nzuri) kutokana na kuwa mafuta mengi yanasababisha kuwa wanene.
Mkondya ambaye ni muasisi wa kijiji cha Nguruwe pia ni mkurugenzi wa Nguruwe Project amesema katika kipindi cha miezi mitatu kijiji hicho kimepokea watalii wa ndani na nje wapatao 1400 kutoka mataifa ya Ugaibuni Zamahero kimepokea ugeni kutoka mataifa ya Uholanzi ,Venezuela ,Ujerumani na Ufaransa,Colombia,Ufilipino, Asia na China pia Watanzania wakitaka kujua sababu iliyomsukuma mfugaji huyo kuanzisha kijiji cha Nguruwe na pia kufahamu tamaduni na changamoto za kuishi na mifugo aina ya nguruwe lakini pia kujifunza na kuwekeza katika kijiji hicho.
Amesema sababu ya kuja na wazo la kijiji cha nguruwe ni kutoa fursa ya ajira pia kwa vijana wengi kuhudumia mifugo hiyo na mifugo mingine kama Kanga na Kuku na kwamba kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya kitoweo cha nyama ya nguruwe ambapo anasema utafiti umeonyesha watu zaidi ya bilioni moja kutoka bara la Africa ni walaji wakubwa wa kitoweo hicho hivyo akaamua kualika wenye nia ya kuwekeza ufugaji wa nguruwe katika kijiji hicho.
Mbali na kuwa kivutio lakini Kijiji cha Nguruwe kimekuwa mkombozi wa ajira kwa vijana akiwemo Haji Mgogo ambaye amepata kazi ya kudumu ya kulisha mifugo,kusafisha mabanda na kutibu pindi magonjwa yanaposhambulia na kisha kupa ahueni katika maisha.
Haji Mgogo ambaye ni miongoni mwa makumi ya wafanyakazi wa kijiji cha Nguruwe wenye jukumu la kulisha mifugo,kusafisha mabanda na kutibu pindi inapougua anasema ajira hiyo imemfanya kujenga kibanda chake na kuendesha maisha tofauti na ilivyokuwa awali alipokuwa hana kazi na kutoa rai kwa vijana kuacha kuchagua kazi.
WASILIANA na Kijiji cha Nguruwe +255 756 000 095
+255 769 300 200
Whatsapp +255 629 300 200
Post a Comment