WAITARA CUP YAENDELEA KUKIWASHA TARIME VIJIJINI

 



                     Na, Ernest Makanya - Tarime.

Michuano ya waitara cup imeendelea kuwa mikali tarime vijijini ambapo kila timu inapania zawadi nono kutoka kwa mbunge wa jimbo la tarime vijijini Mh waitara .

Leo imeendeleaa michezo kadha ambapo zimekutana timu ya Kubiterere FC na Susuni FC na kutoana kwa bao za (3-0)pia mchezo wingine ulio kuwa unaendelea ulikuwa ni baina ya Regicheri Fc na Mwema Fc ambazo pia zimetoa kwa kungana (0-2).


Pia mbunge waitara ameweza kufika viwanjani hapo na kuzungumuza na wachezaji ,viongozi wa timu hizo na kuwataka wadau mbalimbali wa michezo kuendelea kuunga juhudi kwenye hiyo michezo kuhakikisha timu zinafika viwanjani kwa wakati 

Mbunge waitara ameelezaa kuwa michezo inawafanya vijana kuwa( busy ) hivyo kuondokana na makundi mbaya

 

‘Mchezo inayo endelea hapa inawafanya nyie vijana kuwa busy hivyo kujiepusha na makundi yasiyo kuwa mazuri pia mimi kama mbunge kazi yangu ni kupokea matokea sio malalamiko ya uwanjani na ndo maana wakawepo wataalamu wa michezo na hoja yangu kwenu ni kuwambia kuwa munapocheza mjue munacheza ili mpate nini pia zitakuwepo zawadi pia nidhamu inatakiwa kuwepo kwani katika michezo hii tunataka tuunde timu ya jimbo ambayo pia   nina tamani siku moja itoke timu hapa Kwenda kucheza hata na timu ya bunge na pia kupitia michezo hii kuna vijana wataibuliwa na Kwenda kucheza inje ko wito wangu kwa viongozini  kuwashika mkono vijana kwani tunapo kuwa na uhitaji nao wakati wa siasa tunawatumia , na nimefurahi kuwa viongozi mbalimbali wanafutilia  ligi hii kwa ukaribu Zaidi “Amesema Waitara”

Wakati zoezi hilo la michezo likiendelea mbunge waitara ameweza kufika shule ya misingi kubiterere na kushiriki zoezi la utoaji wa msaada kutoka kwa mdau wa maendeleo( Printer)mh mbunge ameunga juhudi hizo kwa kuoa pesa za kitanzania shilingi LAKI MOJA 100,000 kwa ajili ya ununuzi wa rimu paper.



Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA