EWURA YAENDESHA MAFUNZO YA HUDUMA ZA NISHATI NA MAJI KWA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Shinyanga juu ya shughuli za udhibiti wa huduma za nishati na maji kwa lengo la kuimarisha uelewa.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo Alhamisi Mei 2,2024 Mjini Shinyanga, Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Walter Christopher amesema mafunzo hayo ni miongoni mwa hatua zinazochukuliwa na EWURA ili kuhakikisha kuwa umma wa Watanzania unaelewa masuala ya udhibiti na haki na wajibu wao kama watumia huduma za nishati na maji.

Mhandisi Christopher amesema waandishi wa habari ni kundi muhimu na kwamba wakielimishwa vizuri na kuwa na uelewa wa kutosha wataandika habari zao kwa usahihi na kuhabarisha umma.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga, Bw. Patrick Mabula, ameishukuru EWURA kwa semina hiyo na kuahidi elimu watakayoipata wataitumia kuelimisha wananchi kupitia vyombo vyao vya habari.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali vikiwemo magazeti, redio, televisheni na vyombo vya habari vya mtandaoni (Blogs & Online Tv).

Miongoni mwa mada zilizowasilishwa ni pamoja na majukumu na kazi za EWURA na Ofisi ya Kanda ya Magharibi ya EWURA, udhibiti wa masuala ya mafuta na utaratibu wa kuwasilisha malalamiko EWURA.
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na EWURA kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) leo Alhamisi Mei 2,2024 Mjini Shinyanga. Picha na Malunde 1 blog
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na EWURA kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga

Ofisa Uhusiano Mwandamizi EWURA, Tobietha Makafu akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga

Ofisa Mwandamizi Huduma kwa Wateja, EWURA Kanda ya Magharibi Getrude Mbiling’i, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga

Mhandisi Mwandamizi Idara ya Mafuta kutoka EWURA , Ibrahim Kajugusi, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga
Mhandisi Mwandamizi Idara ya Mafuta kutoka EWURA ,Ibrahim Kajugusi, akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA