KAULI YA SERIKALI KWA MBUNGE NDAISABA - SAKATA LA KIKOKOTOO


Na, Mwandishi wetu - Dodoma.

Serikali imesema inatambua umuhimu wa kuboresha mafao ikijumuisha malipo ya Mkupuo kwa wastaafu, Sheria inaitaka Mifuko kufanya tathimini ya kupima uhimilivu kila baada ya miaka mitatu na kutoa ushauri na mapendekezo mbalimbali ikiwemo maboresho ya mafao ya wanachama ambapo kanuni mpya imeanza kutumika mwezi Julai 2022.


Majibu hayo ya serikali yametolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Paschal Katambi kufuatia swali la Mbunge wa Jimbo la Ngara Mheshimiwa Ndaisaba George Ruhoro Leo Mei 10, 2024 Bungeni jijini Dodoma alilouliza kuwa "Je, Serikali ina mpango gani wa kuirekebisha Kanuni ya Kikokotoo ili kuongeza kiwango cha mafao ya mkupuo wa kwanza kwa Wastaafu?" Mhe. Ndaisaba.

 

Naibu Waziri Katambi amebainisha kuwa ni muhimu kuzingatia ushauri wa wataalamu kuhusu uendeshaji, usimamizi na uendelevu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kuwa unazingatia utaalamu wa sayansi ya Watakwimu-bima (actuarial science) na uamuzi wa kubadilisha Kanuni ya Kikokotoo cha Mafao ya Wastaafu ni lazima utokane na tathmini ya kina ya kisayansi ya Watakwimubima kama ilivyoelezwa na Makamu wa Rais wakati wa Sherehe za Mei Mosi.


Majibu hayo ya serikali yakamsimamisha Mbunge Ndaisaba kwa swali la nyongeza akitaka kujua mpango wa serikali kuhakikisha inalipa madeni ya mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuiongezea ukwasi mifuko hiyo na hatimaye iendelee kuwanufaisha wanachama wake.


Aidha serikali hatua iliyochukua "Serikali inawapenda wafanyakazi kwani ndio chachu ya kuleta maendeleo katika kujenga uchumi hivyo baada ya kukuta Kuna madeni ambayo yalikuwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii iliamua kubeba deni hilo na iliendelea kuwalipa wastaafu hao fedha." Amesema Mhe. Katambi


Hata hivyo serikali itaendelea kuhakikisha inaimarisha mifuko hiyo na kuangalia maslahi ya wafanyakazi waliostaafu kwa kulitumikia Taifa kwa uhodari.





Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA