MICHUANO YA WAITARA CUP YATINGA HATUA YA ROBO FAINALI

 


Na, Ernest makanya - Tarime.

Timu  kati ya 16 zilizotinga hatua ya pili katika michuano ya Waitara Cup inayoendelea sehemu mbalimbali za Jimbo la Tarime Vijijini, zimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano hayo, yaliyoanza kurindima mwezi mmoja uliyopita.

Timu hizo ni  Ganyange fc kutoka Kata ya ganyange ,manga fc ya Kata ya manga   kemambo FC ya Kata ya kemambo, Nyamwaga fc ya Kata ya nyamwaga  ,kiore  FC ya Kata ya kiore  , Sirari FC ya Kata ya Sirari, mwema fc ya kata ya mwema na nyasincha fc ya kata ya nyasincha


Timu hizo zimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali katika michuano hiyo baada ya kupata ushindi katika michezo yao ya hatua ya pili na kukamilisha timu nane  zilizofuzu hatua ya tatu (robo fainali) ambazo zitamenyana ili kuwapata washindi watatu ambao wataungana na timu moja kutoka ya mshindwa bora (best loser) kuingia hatua ya nusu Fainali ya mashindano hayo.


Sirari FC wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali kwa mikwaju ya Penati 04 – 03 dhidi ya Matongo FC ambapo ganyange FC walipata ushindi wa mikwaju ya penati 06 – 05 dhidi ya muriba FC na kupata tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali.

Timu nyingine pia lizifanikiwa kutinga hatua ya robo fainal kwa kucheza michezo kama ilivyo kuwa imepagwa na kuibuka washindi na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainal .

Michuano hiyo inadhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mhe. Chief Mwita Mwikwabe Waitara ambapo zawadi za washindi zitakabidhiwa tarehe 09.06.2024 baada ya mchezo wa fainali kumalizika.

 





 

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA