Mr. MANGURUWE AMWAGA TIKETI BURE ZA KWA MASHABIKI SIMBA SC ARUSHA.. AMWITA MANDONGA NA WENZAKE MASHINDANO YA KUBEBA NGURUWE!

 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Kijiji cha Nguruwe kilichopo Zamahero wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma Simon Mnkondya maarufu Mr Manguruwe  amekuja na kali ya kugawa tiketi  bure kwa mashabiki wa soka Mkoani Arusha wapate burudani kwenye mechi ya leo kati ya Simba SC na KMC katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Wakati Mr. Manguruwe akigawa tiketi kwa mashabiki wa Simba SC washabiki wa soka huku wakiibua shangwe na kupiga kelele wakimwita Mr. Manguruwe! Mr. Manguruwe Mr. Manguruwe!! Mr. Manguruweeeeeee!!.

Mr. Manguruwe pia ametangaza kuja na mashindano ya kubeba nguruwe wakubwa wa Zamahero Dodoma na kumkaribisha Mwarabu Faita, Keyoyo , Komando Madafu na Mandonga kuja kujaribu bahati yao ya kubeba nguruwe na endapo mshindani ataweza kubeba nguruwe dume atapata kitita cha milioni 50 sawa na dola 23,000 za Kimarekani.

Wasiliana na M.r Manguruwe 0763755755 na 0767600300.



Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA