Meneja wa kiwanda cha kuchambua Pamba cha Biosustain Co Ltd. kilichopo Mkoani Singida, Salum Salum
Mkurugenzi na mmiliki wa kampuni ya GAKI Investment Ltd. na Makamu mwenyekiti wa makampuni yanayojihusisha na ununuzi na uchambuzi wa Pamba, Gaspar Kileo
****
Kwa nyakati tofauti wamiliki wa Viwanda vinavyochambua zao la Pamba wameonesha kufurahishwa na mpango ambao unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Bodi ya Pamba na wamiliki wa Viwanda vya kuchambua Pamba.
Meneja wa kiwanda cha kuchambua Pamba cha Biosustain Co Ltd. kilichopo Mkoani Singida, Salum Salum amesema mpango wa kutumia maafisa ugani kutoa huduma za ugani katika Kilimo cha zao la Pamba umekuwa na matokeo mazuri kwani uzalishaji umeongezeka kwa maeneo uzalishaji umeongezeka kutoka kilo 300 hadi 800 na 1000 pamoja na mwaka huu 2024 kuwa na mvua nyingi zinazozidi wastani hii ni kutokana na utalaamu unaotolewa.
"Vijana walifika wakati musimu umeanza lakini ushauri wao umeongeza uzalishaji, huu ni mwelekeo mzuri, tumepeleka trekta katika vijiji kumi na vitatiu tumewapa maafisa hawa vitendea kazi na tunatoa mafuta kwa ajili ya pikipiki Kila wiki na wameenda kwa wakulima kila eneo tulilo watumia wako vizuri tumewatumia katika swala la usimamizi katika utendaji wao wako vizuri", amesema Salum.
Meneja huyo ameiomba Wizara ya Kilimo kuwatumia vijana hawa katika ushirika waone namna ya kutumia hii programu ili fedha za wakulima na suala zima la masoko ya pamba yawe na usimamizi mzuri.
Aidha ameshauri kuwa wale ambao hawakuingia katika utaratibu huu wa BBT Ugani msimu huu ujao waingie ili kuondoa usumbufu wa kuingilia wengine kwenye maeneo waliowekeza kwa ajili ya kununua Pamba.
Naye Mkurugenzi na mmiliki wa kampuni ya GAKI Investment Ltd ambayo nayo inajihusisha na ununuzi na uchambuzi wa zao la Pamba ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa makampuni yanayojihusisha na ununuzi na uchambuzi wa Pamba, Gaspar Kileo amewataka wananchi wa maeneo ya mradi kujiandaa kwa msimu ujao kuzalisha zaidi kwani trekta 200 zimeshanunuliwa zitapelekwa vijiji vyote vya mradi wale waliokuwa na wasiwasi waondoe wajiunge ili kuogeza uzalishaji na tija kutoka kupata kilo 1000 kwa eka katika msimu ujao.
Wameyasema hayo wakati walipotembelewa kwenye Viwanda vyao na maafisa kutoka wizara ya Kilimo na Bodi ya Pamba ili kujionea utendaji wa maafisa ugani walio chini ya kampuni hizo.
Post a Comment