Dodoma.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, na Teknolojia imeliomba Bunge kuidhinishiwa jumla ya Tsh.Trillioni Moja, Bilioni Mia tisa Sitini na Nane, Milioni mia mbili kumi na nane na elfu Mia tano na thelathini na nne (1,968,218,534,000.00.) ya Makadirio ya Mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2024/ 2025.
Ombi Hilo limewasilishwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Waziri Prof.Adlf Mkenda alipowasilisha hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25 ambapo amesema ili kuwezesha utekelezaji wa malengo kwa mwaka wa fedha 2024/25, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Fungu 46) inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 1,965,330,380,000.00 kwa mchanganuo ufuatao:
"Wizara kupitia Tume ya Taifa ya UNESCO (Fungu 18) inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 2,882,154,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambapo Mishahara ni Shilingi 1,319,040,000.00 na Matumizi Mengineyo ni Shilingi 1,563,114,000.00." Prof. Mkenda
Post a Comment