Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu,Ujuzi na Ubunifu yamehitimishwa Ijumaa Mei ,31 2024 jijini Tanga.
Maadhimisho hayo yalikuwa yamehusisha vyuo vyote vikuu na vya kati Tanzania, lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa vyuo kuonesha ubunifu wa kutoa Elimu na ujuzi wa kufundisha wanafunzi pindi wawapo vyuoni.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Elimu,Ubunifu na ujuzi,Mkuu wa Chuo cha Afya Kolandoto Shinyanga Paschal Shiluka, amesema maadhimisho ya mwaka huu, yamekuwa kivutio kwa wana Tanga na nchi nzima kwa ujumla kwa kuwa wananchi wamejitokeza kwa wingi.
Amesema kama taasisi ya chuo cha Afya wamenufaika na maadhimisho hayo kwa kujitangaza kwa wananchi wa jiji la Tanga kwa njia mbalimbali, hivyo wanaamini katika mwaka wa masomo 2024/2025 watapokea wanafunzi wengi kutoka ukanda wa Tanga na viunga vyake.
Ametumia nafasi hiyo kuhamasisha wazazi/walezi pamoja na wanafunzi wale wote wenye sifa za kujiunga na fani za afya kwa kuchagua "Kolandoto college of health sciences" wakati wanapotuma maombi ya kujiunga na Chuo kwa kuwa dirisha la usajili sasa lipo wazi.
Kwa upande wake Afisa Habari wa Chuo hicho Josephine Charles ametaja kozi za Afya zinazofundishwa chuoni hapo kuwa ni Uuguzi na Ukunga, Utabibu (Clinical Medicine), Maabara, Famasia, Radiology na Physiotherapy,ambapo amesema kozi za Maabara, Physiotherapy na Radiology zina mkopo wa serikali, hivyo mwanafunzi anaweza omba mkopo kwenye bodi ya mikopo (HELSB) mara baada ya kuomba moja ya kozi hizo.
Pia ameeleza namna ya kujiunga na Chuo hicho kuwa ni kubofya tovuti www.kchs.ac.tz au kupiga simu namba 0742155623 na 0762363826 kisha kufuata maelekezo yote ya kujiunga na Chuo cha sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga.
Aidha maadhimisho ya wiki ya Elimu,Ubunifu na ujuzi yaliyoanza Mei 25, 2024 yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo "Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa uchumi shindani" yamehitimishwa Mei 31 2024 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal jijini Tanga na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambaye alikuwa Mgeni rasmi.
Post a Comment