Na, Ernest Makanya - Tarime.
Timu nne zatinga hatua ya nusu fainal michuano ya Waitara Cup Sirari Fc, Nyamwaga fc, Mwema fc,na Kemambo fc timu hizi zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainal baada ya michezo Yao walio cheza na wapinzani wao na kupata ushindi ulio peleka kufuzu kwenda nusu fainal,michuano ya Waitara Cup inayo endelea kutikisa halmshauri ya Tarime.
Nyamwaga FC waliwakaribisha jirani zao timu ya Ganyange FC kutoka kata ya Ganyange katika mchezo wa hatua ya pili (robo fainali) na kuibuka na ushindi kwa kufunga bao 4 kwa 2 ambayo yamekuwa matokeo ya jumla
Ushindi huo umefanya timu hizo nne kufuzu kwenda hatua ya nusu fainal katika michuano ya Waitara Cup ambayo inafikia tamati tarehe 09.6.2024 kwa mchezo wa fainali utakaochezwa siku hiyo ya fainal na bingwa atakabidhiwa zawadi yake baada ya mchezo huo, kumbuka kuwa michuano hiyo inadhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mhe Chief Mwita Mwikwabe Waitara.
Post a Comment