BALOZI WA MAREKANI AIPONGEZA REDESO KIGOMA KWA USIMAMIZI MZURI MIRADI


Mratibu miradi Redeso Mkoani Kigoma ( wa kwanza kushoto), Balozi wa Marekani nchini Tanzania bwa .Michael Battle( wa pili kutoka kushoto),Mwakilishi UNHCR nchini Tanzania Bi. Mahoua Parums na Mkurugenzi huduma kwa wakimbizi kutoka wizara ya mambo ya ndani nchini Tanzania bw. Soud Mwakibasi (aliyevaa suti nyeusi) wakiangalia maendeleo ya shamba la kilimo hai cha mbogamboga katika kambi ya Nyarugusu Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma leo Julai,26,2024.
Mratibu miradi Redeso Mkoani Kigoma (kushoto), Balozi wa Marekani nchini Tanzania BW.Michael Battle( katikati),Mwakilishi UNHCR nchini Tanzania Bi. Mahoua Parums (kulia) wakisikiliza matumizi ya fedha maelekezo kutoka kwa Mratibu miradi Redeso Kigoma kuhusu shamba la kilimo hai cha mbogamboga katika kambi ya Nyarugusu Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma leo julai,26,2024.

Na Mwandishi wetu - Kigoma

Balozi wa Marekani nchini Tanzania , Michael Battle ametembelea miradi iliyofadhiliwa na serikali ya Marekani kuwahudumia wakimbizi wa kambi ya Nyarugusu na jamii inayozunguka kambi hiyo iliyopo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.

Ziara hiyo amefanya leo Ijumaa Julai 26,2024 kwa kukagua kilimo hai cha mbogamboga kambini hapo huku akishangazwa na fedha chache walizotoa kiasi cha US Dolla 25,000 kunufaisha zaidi ya wakimbizi 250 na wananchi jamii ya wa Tanzania 300.

"Uwekezaji wa fedha kidogo umeonesha inawezekana kutoa taswira nzuri ya kilimo chenye tija haswa kwa kutumia eneo dogo na kuzalisha mbogamboga ambazo ni muhimu kwa afya hasa mmezingatia kundi la watu wenye mahitaji maalumu kuwa wanufaika wa moja kwa moja wa mradi huu,lakini pia mmezingatia mfumo wa matumizi mazuri ya raslimali maji kwenye mradi huu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwenye maeneo yenye changamoto ya maji", amesema Battle.

Mratibu miradi Redeso Mkoani Kigoma bw. Emmanuel Solomoni ameipongeza serikali ya Marekani kwa kuwaamini na kuwapa fedha kwa ajili ya kuwasaidia walengwa na ameahidi kuwa Redeso wapo kuisaidia jamii ya wakimbizi na jamii inayozunguka kwa lengo la kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.


Aidha Mratibu huyo wa Redeso Mkoani Kigoma amesema fedha hizo zimetumika kununua vifaa vya umwagiliaji wa mboga mboga wa matone wa wazi na kuiweka katika shamba la ukubwa wa robo heka katika Kambi ya Nyarugusu, kununua Vifaa vya kitalu Nyumba na kuiweka katika Jamii ya watanzania kata ya Mwilamvya halmashauri ya Mji Kasulu,Kuwafundisha wakulima wadogo wadogo kilimo Cha Bustani ya nyumbani wanufaika 270( 150 watanzania,na 120 wakimbizi huku 80 wakimbizi walio Kambi ya Nyarugusu na 40 wakimbizi wa Kambi ya Nduta.


"Kuwajengea uwezo na kuwawezesha wanufaika 250 kilimo cha umwagiliaji wa Bustani kwa njia ya matone wa wazi wakimbizi 100 wa Kambi ya Nyarugusu na kilimo Cha kitalu Nyumba kwa wanufaika 150 wa Jamii ya watanzania walio katika kata za Mwilamvya na Kigondo , Halmashauri ya Mji Kasulu, Kuwajengea uwezo na kuwawezesha wanufaika 250 ( 100 Jamii ya wamikimbizi wa Nyarugusu na 150 Jamii ya watanzania) katika mbinu za kuzuia opotevu wa mazao ya shambani( post harvest Management),kuhifadhi mazao(Packaging) na kuzitangaza bidhaa zao kwa njia ya (branding)", ameongeza Solomoni.

Solomoni amesema walinunua na kugawa Mbegu za Nyanya,karoti,vitunguu,spinachi,biringanya na Nyanya chungu na zana za umwagiliaji kwa mkono kwa ajili ya kuanzisha Bustani za Mboga mboga katika kaya 120 za watu wenye mahitaji maalumu (Wazee na watu wenye ulemavu wa aina mbali mbali) katika Kambi ya Nyarugusu wanufaika ni 80 huku Kambi ya Nduta(Kibondo) wanufaika wakiwa takribani 40.

Mradi huo ulioanza mwezi october 2023 na unatarajiwa kukamilika Julai 2024 ambapo hadi sasa umetekelezwa kwa asilimia 98.
Kilimo hai cha mbogamboga kwenye kitalu nyumba kilichoko Kata ya Mwilamvya Halmashauri ya Kasulu Mji Mkoani Kigoma mradi unaosimamiwa na Redeso Kigoma kwa ufadhiri wa serikali ya marekani unaotarajiwa kukamilika mwezi Julai 2024
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw.Michael Battle "akigonga tano" (akisalimiana) na watoto wa jamii ya wakimbizi katika kambi la ya Nyarugusu Wilayani Kasulu Mkaoni Kigoma leo Julai 26,2024 alipokuwa akikagua miradi iliyotekelezwa na shirika la Redeso mkoani humo kwa ufadhiri wa ubalozi wa marekani nchini Tanzania.
Mratibu miradi Redeso mkoani Kigoma (wa pili kutoka kulia aliyenyoosha mkono) bw .Emmanuel Solomoni akimwelezea balozi wa Marekani nchini Tanzania (wa kwanza kulia) kuhusu matumizi ya fedha walizopokea kutoka serikali ya marekani.
Mkurugenzi huduma kwa wakimbizi kutoka wizara ya mambo ya ndani nchini Tanzania bw. Soud Mwakibasi akikagua mazao ya mbogamboga katika bustani ya umwagiriaji matone wa wazi.
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA