KESI YA BINTI WA DOVYA KUSIKILIZWA SIKU TANO MFULULIZO - MKUDE AFUNGUKA MAZITO


Na, Mwandishi wetu - Dodoma

 Watuhumiwa wanne wamefikishwa mahakamani kwa thuhuma za kutumwa na afande kumdhalilisha binti wa Yombo Dovya Jijini Dar es salaam Leo Agosti 19, 2024 na kusomewa mashktaka mawili ya kubaka kwa kikundi (gang rape) na kumwingilia kinyume na maumbile binti ambaye hakutajwa jina lake mahakamani.


Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama kuu ya Tanzania Mkoani Dodoma Mkurugenzi msaidizi kutoka Ofisi ya Mashtaka Makao Makuu, Renatus Mkude amesema vijana hao wamekana mashtaka hayo na kutokana na unyeti wa shauri hilo wataendelea kuwa mahabusu huku shauri lao likisikilizwa kwa siku tano mfululizo.


Watuhumiwa hao waliofikishwa mahakamani ni MT. 140105 Clinton Honest Damas maarufu Nyundo,Amin Lord Lema ,Nickson Idala Jackson na C.1693 Playgod Edwin Mushi huku jina la binti aliyefanyiwa ukatili huo kutotajwa mahakamani ili kulinda utu wake kwa mujibu wa sheria za nchi.


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA