Na Mwandishi wetu - Dodoma.
Mgombea aliyeshika nafasi ya pili katika Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Sweetbert Nkuba amekataa kutambua ushindi alioupata mpinzani wake wa karibu Wakili Boniface Mwabukusi kwa madai ya ukiukwaji wa mwenendo wa uchaguzi.
Nkuba ameyazungumza hayo leo Jumamosi Agosti 3,2024 jijini Dodoma saa chache baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo ya uchaguzi wa TLS yaliyomtangaza Mwabukusi kuwa rais mpya aliyepata kura 1,274 akifuatiwa na Nkuba kura 807.
"Matokeo haya yaliyotangazwa siyatambui sababu ya ukiukwaji wa mwenendo wa uchaguzi, tayari nimejipanga na mawakili wangu kwaajili ya kupinga matokeo haya mahakamani," amesema Nkuba.
Post a Comment