AFARIKI DUNIA BAADA YA KUNYWESHWA SUMU NA WATU WANAO JIITA KAMCHAPE



Na, Mwandishi wetu kutoka Katavi.

Busula Magibi Mkazi wa kijiji cha kapalamsenga Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi amefariki dunia baada ya kunyweshwa dawa  inayo dhaniwa kuwa wenda ikawa ni sumu na watu wanaojiita  lambalamba maarufu kamchape wakidai kuondoa uchawi uliopo katika makazi yake.
Ni September 10 ambapo watu walio jiita lambalamba maarufu kamchape walifika nyumbani kwa bi Busula Mabibi Mkazi wa kijiji cha kapalamsenga wakidai wao wamekuja kuondoa kitu cha uchawi  ambacho kipo katika makazi yao

Chales Kalambo ni mtoto wa bi Busula Mabibi ambae alishuhudia chanzo cha kifo cha mama ake amesema ilikua ni mda wa saa 12 jioni kuelekea saa moja walipo maliza kupata chakula cha jioni ndipo dada ake alimpa taarifa kuwa  kuna mtu amesema amekuja kuchapa[Kuondoa uchawi]
Chales amesema alikua mmoja wakaongezeka wakawa watano ndipo walipo mueleza mama ake kuwa kuna kitu kipya cha kichawi kimekuja katika makazi yao hivyo inatakiwa mama huyo apewe dawa  anywe ili wapate ruhusa ya kuingia ndani kuondoa kitu hicho ambacho wali dai kipo katika makazi hayo.

Ameeleza baada ya mama yake kupewa dawa alionekana kuishiwa nguvu huku akidai kujisikia vibaya na kuanza kutoa povu mdomoni na puani alipo fikishwa hospitalini wakaambiwa tayari amekwisha fariki.

Onesimo Buswelu Mkuu wa wilaya hiyo ameitaka familia na wakaazi wa kijiji cha kapala msenga kuwa na moyo wa subila na kutoonyesha hali yeyote ya malumbano ,mafarakano wala ugomvi wakati taratibu za mazishi zikiendelea za kumuhifadhi mama huyo.

Onesimo amebainisha kuwa kulingana na sheria na taratibu za nchi hilo jambo alikubaliki hata kidogo akidai jambo hilo lilijitokeza mwaka jana watu walipoteza mali zao na baadhi ya wanao fanya vitendo hivyo walifikishwa kwenye vyombo vya sheria na wengineo wali hukumiwa jela.

Buswelu ameeleza kuwa watafanya uchunguzi kwa kila kona,ndani ya uvungu na kila sehemu kuhakikisha watu hao wanao jiita kamchape wanaondoka ili kuwahakikishia usalama wananchi wa kijiji hicho.

Amevielekeza vyombo vya dola kuendelea kuwafuatilia walio kimbia na kulishukuru jeshi la polisi kuonyesha ushirikiano na kuwakamata wa watuhumiwa watatu ambao walihusika katika mauaji hayo.

Amewataka wananchi kutoa taarifa pindi wanapo kumbana na mgeni yeyote ili vyombo vya dola viweze kumkamata na kupata maeelezo ya kina kwa mtu huyo.

Wananchi wa kijiji hicho wameiunga mkono kauli ya Mkuu wa wilaya hiyo Onesimo buswelu ya kupambana na vikundi hivyo vinavyo kuja vikijiita kamchape na kuwasababishia vifo vya ndugu, jamaa na marafiki katika eneo hilo.




Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA