Katika jitihada za kuboresha huduma ya maji, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeendelea na zoezi la usomaji mita shirikishi kwa wakazi waliopo ndani ya eneo lake la kihuduma katika Mikoa ya Dar es salaam na Pwani ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Mamlaka kuhakikisha usomaji sahihi wa dira za Maji na kuimarisha mawasiliano
Zoezi hili limeungwa mkono na wakazi wa Mikocheni ambao wamesema kuwa hatua hii itapunguza changamoto za usomaji wa mita na kuomba zoezi hili liwe endelevu.
Ndugu Magreth Mlema mkazi wa mtaa wa Serengeti, Kata ya Mikocheni ameipongeza Mamlaka kwa jitihada za kuhusisha wananchi inaowahudumia katika shughuli zake.
“Ushirikishwaji wa Wananchi katika usomaji mita ni jambo zuri kwani tunaona DAWASA inasikia malalamiko yetu na kusogea karibu kutusikilza na kuyafanyia kazi. Hii inaonyesha ufanisi na uwazi wa hali ya juu niwapongeze kwa hilo na niwasihi zoezi hili liwe endelevu” aliongezea
Zoezi hili pia limeenda sambamba na kutoa elimu juu ya jinsi usomaji mita pamoja na utunzaji wa miundombinu ya maji.
Mkoa wa kihuduma DAWASA Kawe unahudumia takribani wateja 25,000 na unahudumia Kata za Kawe, Mikocheni, Mbezi Juu, Goba, Sinza na Kijitonyama.
Post a Comment