Septemba 30, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Liwale, mbele ya Mhe. Makwaya C. C (Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Liwale), imefunguliwa Kesi ya Jinai Namba 27817/ 2024 ya JAMHURI dhidi ya ZAMOYONI HAJI MMANGO (Mwenyekiti wa Chama cha Msingi Twende Pamoja AMCOS) na RAJAB RASHID NGAIGARA (Katibu wa Chama cha Msingi Twende Pamoja AMCOS).
Washitakiwa wanakabiliwa na kosa moja kwa mujibu wa hati ya mashtaka ambalo ni Kughushi nyaraka kinyume na kifungu cha 333, 335(a) na 337 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16, Marejeo ya Mwaka 2019).
Washitakiwa kwa tarehe tofauti tofauti kati ya tarehe 9, Machi 2022 na tarehe 11, Aprili, 2022 katika Kijiji cha Kitogoro Wilayani Liwale mkoa wa Lindi kwa pamoja na kwa nia ovu ya kuhadaa, walighushi nyaraka ya Tsh. 10,000,000/- (Milioni kumi) yenye kichwa cha habari “ Muhtasari wa Mkutano Mkuu wa Chama Uliofanyika tarehe 09.03.2022" kana kwamba nyaraka hiyo ni halali na imeidhinishwa kwenye Kikao kwa ajili ya mkopo - jambo ambalo washitakiwa walifahamu kuwa sio kweli.
Washitakiwa wote wawili (2)wamekana mashitaka dhidi yao na wapo nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti yaliyotolewa na Mahakama.
Kesi hii inayoendeshwa na Mwendesha Mashitaka Joseph Japhet Emanuel wa TAKUKURU Lindi imepangwa tarehe 21.10. 2024 kwa ajili ya kusikiliza hoja za awali na kuanza kusikilizwa.
Post a Comment