Mnamo tarehe 30/08/2024 imetolewa hukumu ya kesi ya Jinai namba 96/2023 mbele ya Mheshimiwa Hakimu Mkazi Mwandamizi Bittony Mwakisu.Shauri hili liliendeshwa na mawakili wa Serikali Waandamizi Veronica Chimwanda na Fatuma Waziri ambapo mshtakiwa Bw. Bakari Heriel Mchome Afisa Mtendaji wa Mtaa Pugu Kinyamwezi Dar es Salaam, alitiwa hatiani kwa kosa la Kuomba na Kupokea Rushwa ya shs.1,000,000/= (Millioni Moja) kutoka kwa mwananchi ili aweze kumpatia orodha ya majina ya watu waliovamia eneo lake lililopo Pugu Kinyamwezi kinyume na kifungu Cha 15(1) (a) na (2) Cha PCCA [Sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022].
Mshtakiwa amehukumiwa kulipa faini ya sh. 500,000/- au kwenda gerezani miaka mitatu (3). Mshtakiwa amelipa faini.
Habarika & Burudika
Post a Comment