Kijana aliyejulikana kwa jina la Juma Malale (26) mkazi wa Ndembezi Manispaa ya Shinyanga amefariki dunia baada ya kugongwa na Treni.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi Septemba 14,2024 katika eneo la Ubalaji Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa mtu huyo alikuwa ametoka kunywa pombe akalala relini wakati akielekea nyumbani na baada ya treni kufika hapo ilipiga honi lakini hatutoka relini hivyo ajali hiyo ikatokea kutokana na kwamba Treni huwa haisimami.
Hata hivyo bado sababu za Juma Malale ambaye alikuwa anajishughulisha na ujenzi wa nyumba bado hazijajulikana
Post a Comment