UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA WAZIRI MCHENGERWA WAGANGA WAKUU WA MIKOA NYANDA ZA JUU KUSINI WATETA NA WATUMISHI



Waganga wakuu wa mikoa wanaounda kanda ya Nyanda za Juu Kusini wamekutana katika mkutano wa pamoja na watendaji wa sekta ya afya katika kanda hiyo kujadiliana namna bora ya utekelezaji wa masuala mbalimbali katika uboreshaji wa utoaji wa huduma za fya.


Miongoni mwa masuala yaliyogusiwa katika kikao kazi hicho cha Pamoja ni uwajibikaji na usimamizi wa utolewaji wa huduma za afya katika maeneo yao.


Kikao kazi hicho kimewajumuisha waganga wakuu wa Halmashauri, makatibu wa afya wa mikoa na halmashauri, wahasibu wa afya na waratibu wa UKIMWI wa mikoa na halmashauri kutoka katika mikoa minne inayounda kanda hiyo ambayo ni Songwe, Rukwa,Mbeya na Katavi.


Kikao hicho kilichofanyika septemba 04, 2024 ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa aliyoyatoa agosti 31, 2024 akielekeza viongozi kufanya mikutano na watumishi inayojielekeza katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao.


Kikao kazi hicho kimeratibiwa kwa ushirikiano wa waganga wakuu wanne wa mikoa ambao ni Dkt. Ibrahim Isack wa Rukwa, Dkt. Boniface Kasululu wa Songwe, Dkt. Eliza Nyema wa Mbeya na Dkt. Jonathan Budenu wa Katavi.




Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA