WATANZANIA TUMIENI CHUO CHA LIKUYU SEKAMAGANGA-WAZIRI CHANA

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewahamasisha Watanzania kukitumia ipasavyo Chuo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii (CBCTC) Likuyu Sekamaganga kwa kupeleka vijana wapate ujuzi mbalimbali.

Ameyasema hayo leo Septemba 29,2024 alipofanya ziara ya kikazi katika Chuo hicho kilichopo Mkoani Ruvuma.

Amefafanua kuwa chuo hicho ni mahiri katika utoaji wa mafunzo bora ya uhifadhi wa maliasili kwa jamii pamoja na Astashahada na Stashahada ya Utalii na Uongozaji Watalii.

Sambamba na hilo amesema chuo kinatoa Mafunzo kwa Askari Wanyamapori wa Vijiji (Village Game Scouts -VGS) na mafunzo maalum kulingana na mahitaji ya wateja.

"Uzuri wa chuo hiki kipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere hivyo wanaposomea masuala mbalimbali ya Maliasili ni rahisi kufanya mafunzo kwa vitendo" amesisitiza Mhe.Chana.

Chuo hicho kilianzishwa kwa lengo la kuiwezesha jamii kushiriki kikamilifu katika uhifadhi na matumizi endelevu ya Maliasili ili kujiletea maendeleo, kwa kutoa mafunzo stahiki na Ushauri wa kitaalam.
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA