Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi leo Tarehe 28 Oktoba 2024. amempokea mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Monica Chakwera ambaye atakuwepo nchini kushiriki katika Mkutano wa 11 wa Merrick Foundation Africa Asia Luminary, utakaofanyika kuanzia tarehe 29 hadi 30 Oktoba, 2024 katika hotel ya Johari Rotana iliyopo Jijini Dar es salaam.
Mkutano huo unatarajiwa unawakutanisha wenza wa Marais 24 kutoka nchi za Afrika na wengine takriban 500 kutoka nchi mbalimbali Duniani. Mgeni rasmi katika Mkutano huo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.
Post a Comment