TANESCO WATANGAZA KATIZO LA UMEME, WASIOJULIKANA WAWASHA MOTO MASHAMBANI, WANASAKWA

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME

Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mkoani Shinyanga linaomba radhi wateja wake kwa kukosekana kwa huduma ya Umeme katika baadhi ya Maeneo ndani ya Mkoa Wake.

Muda: ni Kuanzia saa 8:15 Usiku Mpaka sasa.

Sababu:  Moto Uliozuka Eneo la Seseko Mashambani na kupelekea nguzo mbili za usafirishaji umeme kuungua na kuanguka.

Maeneo yanayoendelea kuathirika ni

Uzogole, Ning’wa, Chibe, Butengwa, Mwalugoye, Old Shinyanga, Mwalukwa, Pandagichiza, Mwamakaranga, Nindo, Bukambe, Nyamalogo, Shatimba, Mwang’osha, Lyabusalu, Nzumve pamoja na Mwapangabule, Seseko.

Jitihada za Kubadili Nguzo hizo zinaendelea pamoja na kuwatafuta waliosababisha uharibifu huu katika miundombinu ya Umeme.

RAI KWA WANANCHI:  TUNAOMBA WANANCHI WAZINGATIE SWALA LA USALAMA WA MIUNDOMBINU YA UMEME WANAPOENDELEA NA SHUGHULI MBALIMBALI IKIJUMUISHA USAFISHAJI WA MASHAMBA KWANI ULINZI WA MIUNDO MBINU YA UMEME NI JUKUMU LETU SOTE.

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu unaoendelea kujitokeza kutokana na katizo hili.

Tafadhali usiguse wala kukanyaga waya uliokatika, toa taarifa TANESCO kwa simu namba 0748 550 000 au 0733 105 423.

*IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO NA HUDUMA KWA WATEJA TANESCO - SHINYANGA.*

05.10.2024

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA