WANNE WAFARIKI KWA AJALI YA BASI MUDA HUU

 

Na Hamida Kamchalla, KOROGWE.

WATU wanne wamefariki Dunia na wengine 15 kuheruhiwa baada ya basi la abiria la kampuni ya Kaprikoni kuacha njia na kupinduka katika eneo la Mailikumi, wilayani Korogwe.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi amethibitisha na kusema kuwa ajali ilitokea majira ya saa saba na nusu usiku ambapo gari yenye namba T 605 DJR lililikuwa likiendeshwa na Julius Mushi (43) mkazi wa Arusha.


"Tumefuatilia na mpaka sasa waliopoteza maisha ni wanne ambapo wanaume watatu, mwanamke mmoja na wengine 15 wamejeruhiwa, majeruhi wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya (Magunga) lakini wengine wamepelekwa katika hospitali ya rufani ya Bombo" amesema.


Kamanda Mchunguzi ametoa wito kwa madereva kuwa makini wakati wa kuendesha Kwa kufuatia sheria za barabarani Ili kuzuia vifo na majeruhi ambayo vinaweza kudhibitiwa.


"Wakati wote tunawatakaafereva kuchukua tahadhari na kuzingatia sheria za usalama barabarani, udereva ambao unachukua tahadhari wakati wote, waweze making sana wanapoendesha magari yao,


"Kutofuata sheria za barabarani mara nyingi ndio kunapelekea madhara ya uwepo wa ajali yanayotokea ya watu kupoteza maisha lakini vilevile tunaweza kupata majeruhi ambayo yangeweza kuepukika" amesema.


Kaimu Mganga Mfawidhi hospitali ya Korogwe mji (Magunga), Vasco Lucas alisema muda wa saa tisa usiku walipokea majeruhi wa basi hilo wapatao 34 ambao kati yao wanaume 19 na wanawake 14 pamoja na watoto wawili wa kiume ambao wamepata majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili.


Amesema kati ya majeruhi hao, sita walipatiwa rufaa kwa ajili ya matibabu zaidi katika hospitali ya rufani ya Bombo, jijini Tanga lakini pia wamepokea vito vya watu wanne ambao wamehifadhiea katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo.


"Majeruhi waliobaki katika hospitalini hapa ni 27 ambao wanaendelea na uchunguzi na wengine wameshatibiwa na kuruhusiwa baada ya hali zao kuendelea vizuri huku idadi Yao inazidi kupunguza" amesema.


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA