Leo Novemba Mosi, 2024, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, amemsindikiza mke wa Rais wa Jamhuri ya Malawi, Bi. Monica Chakwera katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akirejea nchini Malawi baada ya kuwepo nchini kushiriki Mkutano wa 11 wa Merrick Foundation Africa Asia luminary uliofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 29 Oktoba 2024.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau kutoka katika mataifa mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na wenza wa Marais 15 kutoka katika Bara la Afrika na Asia na kufanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es salaam.
Post a Comment