MHE. LWOTA AWAHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA



Mkuu wa Wilaya ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Kemirembe Lwota leo asubuhi amewaongoza wananchi wa Wilaya ya Serengeti kufanya mazoezi ya viungo katika Mji wa Mugumu.


Akizungumza baada ya kuhitimisha mazoezi hayo Mhe. Lwota amewahamasisha wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika hapa nchini tarehe 27, Novemba, 2024.


Mazoezi hayo ni sehemu ya Serengeti Nyama Choma Utalii Festival inayofanyika leo eneo la Mnadani Mjini Mugumu.



Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA