SACP DKT. DEBORA MAGILIGIMBA ATEULIWA KUWA MJUMBE WA KAMATI YA FEDHA YA IAWP

    

SACP Dkt. Debora Magiligimba

****

Rais wa Shirikisho la Polisi Wanawake Duniani - International Association of Women Police (IAWP), Julia Jaegar, amemteua Kamishna wa Polisi kutoka Tanzania, SACP Dkt. Debora Magiligimba, kuwa mjumbe katika Kamati ya Fedha ya IAWP. 

Hii ni heshima kubwa kwa SACP Dkt. Magiligimba, ambaye sasa atawakilisha Tanzania katika kamati muhimu inayoshughulikia masuala ya kifedha ya IAWP inayolenga kukuza haki, usawa, na maendeleo ya wanawake katika huduma za polisi duniani kote.

Uteuzi wake ni ishara ya imani kubwa kwa uwezo wake katika kuleta maendeleo ya kiutawala na kifedha katika IAWP. 

Kamati ya Fedha ina jukumu la kuhakikisha rasilimali za shirika zinatumika vyema katika kukuza malengo ya IAWP ya kuwasaidia wanawake polisi na kuboresha huduma za polisi duniani.

SACP Dkt. Magiligimba anajiunga na mjumbe mwingine  aliyeteuliwa kutoka Ujerumani katika kamati hii, ambayo ni sehemu muhimu ya usimamizi wa kifedha wa IAWP. 

Uteuzi huu unatoa fursa ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kuongeza ufanisi wa IAWP katika masuala ya kifedha na utawala.

IAWP inatoa jukwaa la wanawake polisi ili kushirikiana, kubadilishana uzoefu, na kusaidiana katika maeneo ya uongozi, mafunzo, na changamoto zinazokumba wanawake katika tasnia ya polisi.

Mbali na uteuzi huu, SACP Dkt. Magiligimba pia alikuwa Mratibu wa Kanda ya 21 wa IAWP (Shirikisho la Kimataifa la Polisi Wanawake), ambapo aliongoza na kuratibu shughuli za polisi wanawake katika nchi 11 za Kusini mwa Afrika. Nchi hizo ni: Tanzania, Angola, Botswana, Eswatini, Lesotho, Malawi, Zimbabwe, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, na Zambia.

Katika nafasi hiyo, alifanya kazi ya kuhamasisha ushirikiano kati ya polisi wanawake katika nchi hizo, na pia alishirikiana kupigania haki za wanawake, na masuala ya kijinsia katika utekelezaji wa sheria  na kuhamasisha polisi wanawake wa nchi hizo 11 kujiunga na IAWP.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA