DKT. KIJAJI AIAGIZA NARCO KUZALISHA MBEGU ZA MIFUGO, MALISHO KWA WINGI

  

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Watatu Kulia) akitoa maagizo kwa NARCO ya Kongwa kukamilisha mradi wa Visima 6 vya maji labla ya Januari 5, 2024 wakati wa Ziara yake leo Disemba 17, 2024
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mwenye Fimbo), akikagua Ng'ombe bora wanaopatikana kwenye Ranchi ya Taifa (NARCO LTD) iliyopo Kongwa, Dodoma Disemba 17, 2024.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji, akisaini kitabu za wageni, mara alipowasili Ranchi ya Kongwa kwa ajili ya Ziara fupi ya Kikazi, Disemba 17, 2024 Kongwa - Dodoma.

◼️Ataka visima 6  vya maji NARCO  Kukamilishwa Kabla ya  January 5, 2025 


Waziri wa Mifugo na  Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameiagiza Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kuongeza wigo wa Uzalishaji wa Mbegu Bora za  Mifugo na Malisho itakayoongeza upatikanaji wa Nyama nchini na Kukuza uchumi wa sekta ya mifugo.

Dkt. Kijaji ametoa maagizo hayo Leo Desemba 17, 2024 Wakati wa Ziara yake kwenye Ranchi ya Kongwa iliyopo Wilayani Kongwa, jijini Dodoma huku akiahidi kurudi Januari 5, 2025 ili kuona utekelezaji wa maagizo yake hayo.
 
" NARCO mnajukumu la kuzalisha mbegu bora za aina Mbalimbali, Watanzania wanahitaji mifugo inayouzika kwa urahisi  hapa ndani ya nchi na  Kimataifa tunataka kila mfugaji akiuza Ng'ombe apate Milioni Nne hivyo nawataka Mzalishe mbegu Bora kwaajili ya wafugaji wetu" amesema Dkt. Kijaji.

Kuhusu uzalishaji wa Mbegu za Malisho Dkt Kijaji amemwagiza Mkurugenzi wa Uzalishaji na Maendeleo ya  Masoko, Stephen Michael  kushirikiana na NARCO kukamilisha malipo ya Mkandarasi wa mradi wa visima sita wenye thamani ya milioni 700 ili visima hivyo vianze kutumika kuzalishia malisho.

" Tumetembelea mradi wa Visima hapa Narco ni mradi mkubwa serikali imetoa milioni 700 lakini umekwama kwa sababu ya madai ya Mkandarasi, sasa nataka nitakaporudi hapa Januari 5, 2025 Visima na Mabirika haya ya kunyweshea Ng'ombe  niyakute yameanza  kutumika" alisema  Dkt. Kijaji.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Bodi ya NARCO, Aziz Mrima  amesema bodi hiyo inajukumu la kuifanya kampuni hiyo kuzalisha  mbegu bora za mifugo zitakazoweza kushindana na wafugaji wengine barani afrika hivyo ameahidi kuyatekeleza  maelekezo ya Waziri Dkt. Kijaji.

Naye Mkurugenzi wa Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko, Stephen Michael  amesema katika kutekeleza maelekezo hayo idara yake itaendelea kufuatilia ili kukamilika mradi huo ambapo hadi sasa tayari Bilioni 3.2 zimepatikana kwaajili ya Malipo hayo.
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA